New York: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan anashinikiza ...
16 Desemba 2003Matangazo
kiongozi wa zamani wa Iraq ahukumiwe kuambatana na sheria za kimataifa."Muimla wa zamani wa Iraq amefanya uhalifu usio na kifani na anastahili kufikishwa mahakamani" amesema hayo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa mjini New-York.Umoja wa mataifa unapinga adhabu ya kifo dhidi ya yeyote yule,hata dhidi ya Sadam Hussein msimamo huo hautabadilika" amesisitiza katibu mkuu Kofi Annan.Kabla ya hapo rais George W. Bush alihakikisha muimla huyo wa zamani atafikishwa mahakamani.Amesema kesi itaambatana na sheria za kimataifa.Akihojiwa na waandishi habari rais George Bush amekwepa kujibu suala kuhusu adhabu ya kifo dhidi ya Saddam Hussein .Dhamana mmoja wa Marekani ambae hakutaka jina lake litajwe amesema Washington haitapinga adhabu ya kifo dhidi ya Sadam Hussein.Balozi wa Marekani anaeshughulikia masuala ya uhalifu wa vita Pierre-Richard Prosper anatazamaiwa kuwasili Baghdad mapema mwakani kuunda korti itakayomhukumu mtawala huyo wa zamani wa Iraq.