New York: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, atafanya...
27 Novemba 2003Matangazo
mazungumzo na kikundi cha washauri wa kimataifa juu ya hatua atakazochukuwa kuhusu Iraq. Ndani ya kikundi hicho cha watu kutoka nchi 16, kutakuwemo wawakilishi wa nchi zote sita zilizo jirani na Iraq pamoja na Misri, na pia wale wa nchi tano zilizo wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na nchi nyingine ambazo ni wanachama wa muda wa baraza hilo, ikiwemo Ujerumani. Kikundi hicho cha washauri kitamsaidia Kofi Annan kuowanisha shughuli za Umoja wa Mataifa katika kuutanzuwa mzozo wa Iraq. Mashauriano ya mwanzo na mabalozi hao wa Umoja wa Mataifa yatafanyika jumatatu ijayo. Ujerumani, Ufaransa na Russia zinataka Umoja wa Mataifa uchukuwe dhamana kubwa zaidi katika kuujenga utawala wa Iraq.