1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpH
ameelezea mwaka 2003 unaomalizika kama ni kipindi kigumu mno katika historia ya miaka 58 ya Umoja wa Mataifa. Katika risala yake ya mwaka mpya, alitangaza mjini New York kuwa ulimwengu unazingatia zaidi vita vya Irak, na hivi sasa unapaswa kuangalia zaidi umaskini, njaa na magonjwa ya hatari duniani. Katika mwaka 2004 Jumuiya ya Kimataifa ikabiliane na vitisho vinavyowakabili wakaazi billioni kama tatu duniani, - alitamka Annan. Bila ya Maendeleo na Matumaini, hapatakuwapo amani duniani, - alisema Annan.