1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kikosi cha Umoja wa Afrika kwenda Somalia

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQ4

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kwa pamoja kikosi cha Umoja wa Afrika kusaidia kuidumisha Somalia katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Azimio lililopitishwa na baraza hilo linazihimiza nchi 53 za Afrika kutoa wanajeshi katika kikosi cha wanajeshi 8,000 cha Umoja wa Afrika. Azimio hilo pia linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zitoe misaada ya kifedha na misaada mingine.

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huenda kikaenda Somalia kuchukua nafasi ya kikosi cha Umoja wa Afrika baada ya miezi sita kumalizika.

Hapo jana watu takriban 12 waliuwawa mjini Mogadishu kufuatia mapigano makali kati ya vikosi vya usalama na watu wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu.

Mapigano hayo yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea mjini Mogadishu tangu serikali ya mpito ya Somalia ikisadiwa na majeshi ya Ethiopia ilipofaulu kuwafurusha wanamgambo wa mahakama za kiislamu kutoka mjini humo mwishoni mwa mwaka jana.