1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Kofi Annan amtaka rais wa Iran kumwacha huru mwandishi.

20 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjG

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amemtaka rais mpya wa Iran Mahmoud Ahmedinejad kumuacha huru mwandishi habri Akbar Ganji kwa misingi ya kibinadamu.

Barua ya Bwana Annan inakuwa ni hatua ya kwanza kubwa ya taasisi hiyo ya kimataifa katika kutafuta njia ya kuachiwa kwa Ganji.

Mapema wiki hii, Ganji aliacha mgomo wake wa kula uliochukua siku 60 akipinga hukumu yake ya kifungo.

Alifungwa jela mwaka 2000 na kuhukumiwa kifungo cha miaka sita , kwa kuhatarisha usalama wa nchi pamoja na makosa mengine.

Kukamatwa kwake kunafuatia kuandika taarifa mbali mbali zinazowahusisha maafisa wa ngazi za juu na mauaji ya wapinzani kadha wa kisiasa.