1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK Kofi Annan ataka mauaji ya Darfur yakomeshwe.

17 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFd3

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amelitolea wito baraza la usalama la umoja huo kuyakomesha mauaji na uharibifu unaoendelea katika eneo la Darfur nchini Sudan. Ameileza hali ya Darfur kuwa mbaya mno na kuilinganisha na jehanamu. Katika miaka miwili iliyopita, wanamgambo wa janjaweed wamewaua raia elfu 70 na wengine zaidi ya milioni mbili kulazimika kuyahama makazi yao. Annan amesema analiunga mkono azimio la Marekani linalopendekeza kufungiwa raslimali na usafiri kwa wale watakaoukiuka mkataba wa kusitisha mapigano ya Darfur. Akiwa pamoja na kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa, Louse Arbour, Annan amesema waliohusika katika uhalifu wa kivita huko Darfur wanastahili kushtakiwa kwenye mahakama kuu ya kimataifa, utaratibu unaopingwa na Marekani.