New York. Lamy kuwa mkurugenzi mpya WTO.
14 Mei 2005Matangazo
Kamishna wa zamani wa biashara katika jumuiya ya Ulaya Bwana Pascal Lamy anatarajiwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la biashara duniani WTO, baada ya mpinzani wake pekee wa mwisho kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.
Mwanadiplomasia kutoka Uruguay Carlos Perez del Castillo, ametangaza kujiondoa baada ya baraza maalum la uteuzi kusema kuwa Bwana Lamy anaungwa mkono kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wanachama 148 wa WTO. Wagombea wengine wawili walijondoa mapema.
Lamy anachukua nafasi inayoachwa wazi na mkurugenzi wa sasa wa WTO Supachai Panitchapakdi kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Septemba mwaka huu.