1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Russia na China zalipigia kura ya turufu azimio kuhusu Burma.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCb0

Russia na China zimepiga kura ya turufu dhidi ya azimio lililolenga kumaliza ukandamizaji wa kisiasa nchini Burma.

Nchi hizo, ambazo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zililipinga azimio hilo zikisema ingekuwa bora kuwataka watawala wa kijeshi wa Burma kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa na kukabiliana na vitendo vya ubakaji vinavyotekelezwa na majeshi ya nchi hiyo.

Hiyo ndio mara ya kwanza tangu miaka ishirini iliyopita, ambapo kura mbili za turufu zimetumiwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuna wafungwa wa kisiasa zaidi ya elfu moja nchini Burma.

Mwanasiasa mtetezi wa demokrasia ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Nobel, Aung San Suu Kyi anazuliwa nyumbani.

Mwaka elfu moja mia tisa na tisini, Chama cha National League for Democracy kinachoongozwa na Bi Aung San Suu Kyi kilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu lakini hakijapewa nafasi ya kuingia madarakani.