1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK: Taasisi ya Bill Clinton yashawishi mashirika ya magharibi kupunguza bei ya madawa na mitambo ya kupima ukimwi-

15 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFj8
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, amesema taasisi yake imefikia makubaliano na mashirika matano makubwa, yanayotengeneza madawa na mitambo ya kupima ikiwa mtu ana virusi vya HIV, vinavyosababisha ukimwi. Bwana Bill Clinton amesema mashirika hayo yamekubali kupunguza bei kwa kiwango cha asilimia themanini, hatua ambayo itaziwezesha nchi masikini kupata mafanikio zaidi katika vita dhidi ya ugonjwa huo hatari. Nchi za kwanza zitakazofaidika na hatua hiyo, ni nchi za bara la Afrika, zilizoanzisha ushirikiano na taasisi ya Bwana Bill Clinton. Nazo ni Msumbiji, Rwanda, Afrika ya kusini, na Tanzania. Katika nchi hizo wanaishi zaidi ya asilimia thelathini na tatu ya watu wote wanaoishi na virusi vya ukimwi barani Afrika.