1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York: Umoja wa Afrika,AU, unawasilisha mpango wake wa kulifanyia marekebisho Baraza la Usalamala Umoja wa Mataifa

19 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEst

Umoja wa Afrika, AU, umewasilisha mswaada wa azimio mbele ya Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa juu ya kupanuliwa baraza la usalama la umoja huo. Mwakilishi wa Nigeria, Aminu Bashir Wali, aliyewasilisha mswaada huo, alisema huo ndio msingi wa mashauriano na nchi nyingine wanachama pamoja na makundi yalio na maslahi. Pindi mswaada huo utakubaliwa, basi baraza la usalama litapanuliwa kutoka wanachama 15 wa sasa na kufikia 26. Wanachama sita wepya wa kudumu watakuwa na kura za turufu. Mswaada mwengine uliowasilishwa na Ujerumani, Japan, Brazil na India unataka baraza la usalama liwe na wanachama 25, kukiwemo wanachama sita wa kudumu ambao hawatakuwa na kura za turufu. Mashauriano ya kufikia suluhu baina ya mapendekezo hayo mawili yanaendelea.