1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa waidhinisha mkataba wa biashara ya silaha uandaliwe

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyn

Kamati ya Umoja ya Mataifa imeidhinisha kazi ya kuandaa mkataba wa kimataifa wa biashara ya silaha. Hatua hiyo italenga kuondoa matatizo yaliyopo katika sheria za sasa zinazoruhusu bunduki zipelekwe katika maeneo ya mizozo licha ya kuwepo kwa vikwazo vya silaha.

Wanachama 139 wa Umoja wa Mataifa wameuunga mkono mswada huo. Marekani ni nchi pekee iliyoupinga mswada huo. China na Urusi hazikupiga kura.

Wadadisi wanasema ingawa huenda ichukue miaka kadhaa kabla mkataba huo kuanza kufanya kazi, uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuruhusu mkataba mkataba utayarishwe ni hatua muhimu katika kauanisha biashara ya silaha duniani.