NEW YORK : Umoja wa Mataifa yaonya dhidi ya jaribio la nuklea la Korea Kaskazini
7 Mei 2005Kiongozi wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya nuklea amesema viongozi wa dunia wanatakiwa kuishinikiza Korea Kaskazini kutofanya jaribio la silaha za nuklea.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu Mohammed El Baradei amewaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba madhara ya kisiasa na kimazingira ya jaribio hilo yatakuwa ya maafa makubwa. Alikuwa akizungumza pembezoni mwa mkutano uliodhaminiwa na Umoja wa Mataifa juu ya mkataba wa kuzuwiya kuenea kwa silaha za nuklea.
El Baradei pia amesema hali hiyo ya Korea Kaskazini ni ya dharura kwa kuzingatia repoti za ujasusi za hivi karibuni kwamba serikali ya Pyongyang yumkini ikawa inajiandaa kufanya jaribio la nuklea.