1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. UN na AU zafikia makubaliano kuhusu Darfur.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu5

Umoja wa mataifa na umoja wa Afrika wamefikia makubaliano kuhusu jeshi litakalokuwa na wanajeshi 23,000 la kulinda amani katika jimbo la Darfur.

Hata hivyo hawajaweza kupata suluhisho kuhusu nani atakuwa na udhibiti wa operesheni hiyo.

Makubaliano hayo, ambayo yamo katika ripoti iliyopelekwa katika baraza la usalama la umoja wa mataifa , inahitaji hata hivyo kuidhinishwa na kamati ya amani na usalama ya umoja wa Afrika pamoja na baraza lake.

Wakati huo huo kundi la kimataifa linalotetea haki za binadamu Amnesty International limezindua tovuti inayohusu watu kuweza kuona picha za satalite za vijiji katika jimbo la Sudan la Darfur. Kundi hilo linamatumaini kuwa tovuti hiyo itasaidia kuzuwia ukiukaji wa haki za binadamu na kuleta uwelewa kuhusu jimbo hilo lililokumbwa na mizozo.