1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Viongozi wa Israel na Palestina kukutana New York mwezi huu.

4 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEeU

Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa mwezi huu mjini New York.

Gazeti la kila siku la Israel Haaretz limesema kuwa viongozi hao wawili watakutana wakati wa kikao cha baraza kuu la umoja wa mataifa. Hapo kabla Mahmoud Abbas amesema kuwa mazungumzo ya kuleta amani mashariki ya kati yanapaswa kuanza haraka baada ya Israel kukamilisha zoezi la kuwaondoa walowezi wa Kiyahudi kutoka katika eneo la Gaza, zoezi zinalotarajiwa kukamilika katikati ya mwezi wa Septemba.

Katika mahojiano , Abbas amesema kuwa anamatumaini kuwa taifa la wapalestina litaanzishwa ifikapo mwaka ujao.

Pia ameahidi kuyaleta makundi tofauti ya wanamgambo yanayohusiana na wanaharakati wa chama tawala cha Fatah chini ya udhibiti wa pamoja katika muda wa wiki tatu.