NEW YORK:Daimler Chrysler and Siemens yatajwa katika ripoti ya kashfa.
28 Oktoba 2005Matangazo
Ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya mpango wa kununua chakula kutokana na mauzo ya mafuta nchini Irak,imelitaja jina la kampuni ya Daimler-Chyrsler na Siemens kuwa miongoni mwa makampuni zaidi ya alfu 2 yaliyohusika na ubabaifu juu ya mpango huo.
Uchuguzi wa Umoja wa Mataifa umeonyesha kwamba makampuni katika nchi 66 yalitoa magendo kiasi cha dola bilioni 1 na nukta nane kwa serikali ya Saddam Hussein.