NEWYORK: Iran na Korea Kaskazini zatuwama kwenye mkutano wa kuzuia kuunda silaha za Nuklea
3 Mei 2005Matangazo
Ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa 188 juu ya kuzuia mashindano ya kuunda silaha za nuklea mjini New York hapo jana ulituwama kwenye nia ya kuunda silaha za nuklea katika mataifa ya Iran na Korea Kaskazini.
Katika mkutano huo utakaochukua takriban muda wa mwezi mmoja kumalizika,Marekani imetaka mkataba huo wa mwaka 1975 uhakikishe Tehran pamoja na Pyong yang ziwekewe ngumu katika mipango yao ya kufaidika na silaha za Nuklea kutokana na kukiuka sheria ya mkataba huo.
Mkuu wa shirika la kimataifa linaloshughukia masuala ya nguvu za Atomiki Mohammed Elbaradei ameitolea wito Iran kutorejelea upya mpango wake wa kuten