New_York: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ameshauri kikosi ...
10 Januari 2004Matangazo
cha wanajeshi zaidi ya elfu sita wa umoja wa mataifa kitumwe nchini Ivory Coast.Katika ripoti yake kwa baraza la usalama,katibu mkuu Annan amesema kikosi hicho kitakua na jukumu la kusimamia usalama katika maeneo yaliyotengwa kuambatana na makaubaliano ya kuweka chini silaha.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amesema ndani ya ripoti hiyo wanajeshi wa Umoja wa mataifa watakua na jukumu pia la kusimamia makubaliano ya kuweka chini silaha,na kuingilia kati ikilazimika.Kikosi kipya cha umoja wa mataifa kitawajumuisha pia wanajeshi 1400 wa jumuia ya ushirikianowa kiuchumi Afrika magharibi-Ecowas walioko nchini Ivory Coast.Katibu mkuu Kofi Annan ameshauri kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa kitumwe february nne ijayo-tarehe ya kumalizika muda wa shughuli za kikosi cha Umoja wa mataifa Minuc vikosi vya Ufaransa na Ecowas pia nchini Ivory Coast.Wakati huo huo waziri mkuu wa Ivory Coast Seydou Diarra amefungua rasmi opereshini ya kupokonywa silaha makundi yanayohusika na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.