Matangazo
Nchini Afrika ya Kusini, visa vya chuki hata mauwaji ya raia wa kigeni kutoka mataifa ya kiafrika na Asia, vimekuwa sugu. Licha ya kuweko tangu Machi 2019 sheria mpya ya kupambana na ubaguzi na chuki dhidi ya wageni, serikali ya Afrika ya kusini bado haijatekeleza kikamilifu sheria hiyo ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria raia wa kawaida, maafisa wa polisi au hata maafisa wa serikali wanaohusika na vitendo hivyo. Katika makala ya Mbiu ya Mnyonge tunaangazia kwa nini mashambulio ya ubaguzi yanajirudia nchini Afrika ya Kusini. Kupitia DW msimulizi wako ni mimi Saleh Mwanamilongo, Karibu.