1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NIAMEY: Annan atembelea eneo la njaa nchini Niger

25 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEi0

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amekutana na viongozi wa Niger-nchi iliyokumbwa na ukame.Lengo la ziara ya Katibu Mkuu Annan ni kusisitiza mzozo wa chakula katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.Annan amesema Umoja wa Mataifa umedhamiria kuwapatia msaada wote wanaohitaji msaada nchini Niger.Vile vile amezunguza juu ya hatua za kuchukuliwa hivi sasa na baadae kuhakikisha kuwa hali kama hii haitotokea tena katika siku zijazo.Siku moja kabla ya ziara ya Annan,kikundi cha Kifaransa kinachotoa misaada-MSF,kilitoa lawama dhidi ya Umoja wa Mataifa kwa kusema kuwa Umoja huo ulichelewa kuchukua hatua kuhusu mzozo wa hivi sasa na hata hatua zinazochukuliwa bado hazitoshi.Zaidi ya watu milioni 2.5 wanakabiliwa na upungufu wa chakula nchini Niger kwa sababu ya ukame na nzige walioteketeza mashamba.