1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger yafuta leseni, shirika la Acted la Ufaransa

13 Novemba 2024

Utawala wa kijeshi nchini Niger umeifuta leseni ya shirika lisilo la kiserikali la Acted la Ufaransa. Shirika hilo sasa halitaweza kufanya kazi nchini humo

https://p.dw.com/p/4mwwI
Kumekuwa na mvutano kati ya Niger na Ufaransa
Kumekuwa na mvutano katika miaka ya hivi karibuni kati ya Niger na Ufaransa, mtawala wa kikoloni wa zamani wa Niger.Picha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Hatua hiyo imechukuliwa wakati ambapo kuna mvutano kati ya serikali ya Niger na Ufaransa ambayo ni mtawala wake wa kikoloni.

Shirika hilo Ufaransa limekuwa likifanya kazi nchini Niger tangu mwaka 2009, likijishughulisha zaidi na watu waliokimbia makazi yao katika taifa hilo lililokumbwa na ghasia za waasi.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Niger ilitoa taarifa hiyo, bila ya kueleza sababu za kufuta leseni hiyo. Shirika jingine la APBE pia lilikumbwa na kadhia kama hiyo ya kufutiwa leseni.

Tangu utawala wa kijeshi ulipoingia madarakani Julai 2023, ulianza kuipa kisogo Ufaransa, na kuanzisha uhusiano na wanaharakati wenzao Burkina Faso na Mali, pamoja na Urusi.