1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria kuanza kulegeza vizuwizi vya kutoka nje

Sekione Kitojo
28 Aprili 2020

Nigeria  itaanza  kulegeza  hatua za kuwazuwia  watu kutoka nje  iliyowekwa katika  miji ya  Lagos  na  mji  mkuu Abuja  kuanzia  Mei 4, rais Muhammadu Buhari  amesema jana  jioni.

https://p.dw.com/p/3bVjE
Nigeria Coronavirus Polizei Kontrolle
Picha: Getty Images/P.U. Ekpei

Buhari  alisema  katika   hotuba kwa njia  ya  televisheni kuwa  ameaidhinisha  awamu za kulegeza  taratibu  hatua za  kuzuwia  watu  kutoka  majumbani  mwao.

Amewasilisha  hatua  mpya  ikiwa  ni  pamoja  na  amri ya kutotoka  nje  usiku, ulazima wa  kuvaa  barakoa  na kupigwa  marufuku  safari zisizo  za  lazima  kati ya majimbo tofauti.

Pia  ametangaza  kufungwa  kwa  muda  wa  wiki  mbili  mji mkubwa  upande wa  kaskazini  mwa  Nigeria  wa  Kano baada  ya  maafisa  kusema  wanachunguza  ongezeko la vifo vinavyoshangaza.

Zaidi ya  watu  milioni 25  mjini Abuja, Lagos  na  jimbo  jirani  la  Ogun  wamekuwa  katika hatua ya  kuzuiwa  kutoka  nje  tangu Machi 30  pamoja  na majimbo  mengine  wameanzisha  amri  zao  za  vizuwizi.