Nigeria yaadhimisha miaka 50 ya uhuru
1 Oktoba 2010Matangazo
Nigeria leo inatimiza miaka 50 tokea ilipopata uhuru wake mwaka 1960.Nchi hiyo iliyoko magharibi mwa Afrika, ni miongoni mwa nchi zenye nguvu kubwa kiuchumi barani humo.Na wakati nchi hiyo ikiadhimisha miaka hiyo 50 ya uhuru wake kundi moja maarufu la wanamgambo katika eneo la Delta nchini humo limeonya kutokea kwa milipuko.Hata hivyo kama alivyonifahamisha Katibu Mkuu wa zamani wa uliyokuwa umoja wa nchi huru za kiafrika OAU Dr Salim Ahmed Salim Nigeria imebakia kuwa nchi muhimu kwa bara la Afrika na wananchi wake kwa ujumla.
Mwandishi:Aboubakary Liongo
Mhariri:Josephat Charo