1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yaaga Kombe la Dunia la Wanawake

7 Agosti 2023

Timu ya Soka ya Wanawake ya Nigeria imeyaaga mashindano ya Kombe la Dunia leo baada ya kupoteza mchezo wake wa hatua ya mtoano dhidi ya England ulioamualiwa kwa mikwaju ya penalti.

https://p.dw.com/p/4Ur6m
WWCup Nigeria vs England
Picha: Tertius Pickard/AP/picture alliance

Kwenye mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita, England imejikatia tiketi ya kusonga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa penati 4 kwa 2 mbele ya timu ya Nigeria inayofahamika kwa jina la utani la "Tai Wakubwa". 

Soma zaidi: Nigeria yaiangusha Ireland Kombe la Dunia la Wanawake
Ufaransa yaishindilia Italia 5 - 1

Kuondolewa kwa Nigeria kumefifisha matumaini ya bara la Afrika kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Australia na New Zealand baada ya hapo jana wawakilishi wengine wa bara hilo timu ya soka ya Afrika Kusini kuyaaga mashindano hayo. 

Banyana Banyana walilazimishwa kichapo cha bao 2-0 kwenye mtanange wao dhidi ya Uholanzi.

Hivi sasa Morocco ndiyo wawakilishi pekee wa bara hilo waliosalia na watajitupa uwanjani hapo kesho kuikabili Ufaransa.