1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yachoma tani 4 za magamba ya kakakuona

17 Oktoba 2023

Nigeria imechoma tani nne za magamba ya kakakuona yaliyokamatwa ya thamani ya dola milioni 1.4, ikiwa ni mara ya kwanza kuharibu hadharani bidhaa za wanyama pori zilizokamatwa kwa lengo la kudhibiti ulanguzi usio halali.

https://p.dw.com/p/4XeIm
 Dokumentation Schuppentiere in Not - Geschäfte mit einer bedrohten Art
Magamba ya kakakuona.Picha: Java

Aliyu Jauro, mkurugenzi mkuu wa wakala wa kitaifa unaosimamia sheria na viwango vya ubora wa mazingira na utekelezaji wake (NESREA), amewaambia waandishi habari mjini Abuja baada ya operesheni hiyo ya siku ya Jumatatu (Oktoba 16) kwamba kuharibiwa kwa vitu hivyo vilivyokamatwa ni ujumbe mzito kuhusu ari yao ya kuyalinda mazingira, wanyamapori na kupambana na biashara haramu inayohatarisha aina ya viumbe kutoweka katika uso wa dunia.

Nigeria imekuwa njia kuu ya upitishaji wa magamba ya kakakuona wa Afrika na bidhaa nyingine za wanyamapori zinazosafirishwa kupelekwa barani Asia.