1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yafungwa na Ugiriki na kukalia kuti kavu

Aboubakary Jumaa Liongo17 Juni 2010

Nigeria imejiweka katika nafasi ngumu ya kufuzu kwa raundi ya pili ya michuano ya fainali za kombe la dunia baada ya kufungwa mabao 2-1 na Ugiriki katika mechi za kundi B.

https://p.dw.com/p/NtwW
Beki wa Nigeria Sani Kaita akitoka nje baada ya akupewa kadi nyekundu kwa kosa la kizembePicha: AP

Kwa kipigo hicho cha sasa Nigeria inalazimika kuigunga Korea Kusini mwa mabao mawili na wakati huo huo ikiombea Argentina iifunge Ugiriki bila ya wavu wake kutikiswa.

Nigeria ilikuwa ya kwanza kufunga kwa bao la Kalu Kaita katika dakika ya 16, lakini Ugiriki walisawazisha bao hilo kupitia kwa Dimitris Salpingidis katika dakika ya 44, kabla ya Vassilis Torosidis kupachika la pili katika dakika ya 71.Kutolewa kwa beki wa Nigeria Sani Kaita kwa kosa la kizembe kulichangia Nigeria kushindwa mchezo huo.

Mapema Argentina ilikuwa nchi ya kwanza kufuzu kwa raundi ya pili baada ya kuifunga Korea Kusini mabao 4-1.

Mwandishi:Aboubakary Liongo