Nigeria yatolewa Kombe la Mataifa ya Afrika
20 Novemba 2014Ikihitaji ushindi ili kupata fursa ya kulitetea taji lake ililolinyakuwa nchini Afrika Kusini mwaka jana,Nigeria ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini katika mpambano huo uliochezwa katika mji wa Uyo nchini Nigeria,magoli ambayo yaliwekwa wavuni na Tokelo Rantie.
Nigeria ilisawazisha magoli hayo dakika za mwisho mbele ya mashabiki wa nyumbani waliokuwa wakitapia ushindi lakini ushindi wa Jamhuri ya Congo katika michuano ya kundi A nchini Sudan umekuwa wa mshangao mkubwa na moja kwa moja kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya pili nyuma ya Afrikas Kusini katika kundi lao.
Mabingwa hao wa Afrika walikuwa na kajimatumaini fulani wakati timu hiyo ya Sone Aluko ilipopachika bao dakika ya 69 kufuatia mkwaju uligonga mwamba na kurudi. Aliko alisawazisha bao la pili katika dakika za majeruhi lakini timu hiyo ya Nigeria ikashindwa kuambulia ushindi.
Misri kwenye mkosi tena
Ivory Coast,Ghana na Mali ingawa zilichelewa kufuzu michuano hiyo zimeweza kuingia kwenye fainali za michuano hiyo itakayofanyika Equatorial Guinea hapo mwezi wa Januari na Februari mwakani.
Baa lililoikumba Misri hivi karibuni limeendelea baada ya timu hiyo kushinda bao 1-0 dhidi ya Tunisia na hiyo kushindwa kwa mara ya tatu mfululizo kuingia katika fainali za Kombe la Afrika kutokana kupoteza mchezo huo kwa mabao ya jumla ya 2-1.
Misri ilitakiwa ishinde kwa mabao 2 ili kuingia katika fainali hizo na kuwa ushindi wake wa kwanza kufuzu fainali hizo tokea ilinyakuwe Kombe la Mataifa ya Afrika hapo mwaka 2010.
Kushindwa kwa timu hiyo na Tunisia ambayo tayari ilikuwa imejipatia tiketi ya kushiriki fainali za michuano hiyo inamaanisha kwamba Congo imechukuwa nafasi ya mwisho ikiwa kama timu bora ya mwisho kwenye makundi yote saba.
Guinea ilioathirika na Ebola yafuzu
Ivory Coast ilijipatia pointi iliokuwa ikiihitaji baada ya kutoka sare ya 0-0 na Cameroon iliokuwa na wachezaji 10 na kushika nafasi ya pili baada ya Cameroon katika michuano ya kundi D. Mashabiki waliuvamia uwanja wa Abidjan kufuatia kufuzu kwa timu yao na kulizuka purukushani na polisi wakati mashabiki hao walipojaribu kuwakumbatia wachezaji.
Ghana nayo ilishinda Togo mabao 3-1 kujihakikishia kushiriki fainali wakati Mali ambayo ilishiriki nusu fainali mbili zilizopita za michuano hiyo zilikwepwa kutolewa katika mchuano hii baada ya kukomesha ushindi wa michezo mitano wa Algeria katika kundi B kwa kuilaza timu hiyo kwa mabao 2-0 huko Bamako.
Guinea timu ilioathirika na ugonjwa wa Ebola imeingia fainali baada ya kuishinda Uganda kwa mabao 2-0 katika uwanja mtupu huko Casablanca Morocco.Guinea ilipigwa marufuku kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya kuwania kufuzu fainali kwa sababu ya Ebola na timu hiyo ilikuwa haina wafuasi wa kuishangilia wakati ilipojipatia ushindi huo.
Wenyeji wa michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Equatorial Guinea,timu ilioko daraja la juu ya Afrika yaani Algeria,Cape Verde,Tunisia,Afrika Kusini,Zambia, Cameroon,Burkina Faso,Gabon na Senegal tayari zimefuzu kuinngia kwenye fainali hizo kabla ya michuano ya Jumatano.
Ratiba ya michuano ya fainali hizo za Kombe la Mataifa ya Afrika inatazamiwa kutangazwa Desemba 3.
Mwandishi : Mohamed Dahman/ AFP
Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman