Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, anasema anaamini atarejea Tanzania kuendeleza kile alichokuwa akikipigania na anachoamini kuwa kilisababisha kushambuliwa kwa risasi miezi mitatu iliyopita akiwa nyumbani kwake, Dodoma, makao makuu ya taifa hilo la Afrika Mashariki.