Njia 10 zinazonyesha ugonjwa wa Malaria ni hatari duniani
21 Agosti 2019Siku ya Malaria duniani ambayo ni tarehe 25 mwezi wa Agosti inatumika kuadhimisha ugunduzi wa mwaka 1897 uliofanywa na daktari wa Uingereza Ronald Ross kuwa mbu wa kike ndio wanaoambukiza ugonjwa wa Malaria kati ya binaadamu, lakini shirika la afya Ulimwenguni WHO linaonya hatua za kupambana na ugonjwa huo zinakwama.
Hizi ndio njia kumi ambazo mbu wamewaathiri binaadamu.
1. Aina nyingi za mbu zinanyonya damu ya binaamamu na kuwapa aina ya kirusi kinachoitwa pathogen, hii ikimaanisha kuwa mbu huyo akikuuma anaweza moja kwa moja kukuambukiza ugonjwa wa Malaria. Na hii ndio sababu inayowafanya mbu kuwa moja ya wadudu hatari duniani.
2. Malaria inasababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja kila mwaka huku shirika la afya ulimwenguni likionya nusu ya idadi ya watu duniani ipo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo. Mwaka 2017 Malaria ilisababisha vifo 435,000.
3. Asilimia 90 ya vifo vitokanavyo na Malaria vinatokea barani Afrika, na kwa sasa nchini Burundi nusu ya idadi ya watu nchini humo wameambukizwa.
4. Visa vya Malaria vinaendelea kusambaa katika mataifa tofauti ikiwemo Uganda ambako wizara ya afya imetangaza ongezeko la asilimia 40 la ugonjwa huo mwaka huu.
5. Ugonjwa wa Dengue unaosababishwa pia na mbu unatokea katika maeneo yaliyo na ukame ambapo watu milioni 2.5 wapo katika hatari ya kuambukizwa.Takriban visa milioni 100 vipya vya ugonjwa huo vinakadiriwa kutokea kila mwaka katika zaidi ya mataifa 100.
6. Mbu kwa kawaida wanapaa umbali wa mita 400. Aina ya mbu wanaoambukiza ugonjwa wa Zika wanazaana katika matairi ya magari, makopo ya bati, makopo ya mbwa na vyombo vya udongo vya kuwekea maua.
7. Baada ya ugonjwa huo wa Zika kusambaa nchini Marekani mwaka 2016 wataalamu walionya kuwa magonjwa mengi hatari yanaweza kutokea katika maeneo makavu.
8. Zaidi ya watu bilioni moja wakiwemo wale walioko nchini Marekani, na barani Ulaya wanaweza kufikiwa na virusi vinavosambazwa na mbu ifikapo mwaka 2080 iwapo hali ya joto itaendelea kushuhudiwa, hii ikiwa ni kulingana na utafiti uliyofanwa na kutolewa mapema mwaka huu na shirika moja la Marekani.
9. Kama umekuwa ukijiuliza ni kwanini Mbu wanawazowea tu watu wa aina fulani, utafiti uliyochapishwa katika jarida la afya la PNAS unasema kwamba baadhi ya watu hawatoi harufu ya aina fulani inayowafukuza mbu.
10. Jinsi ya kuwaangamiza mbu, njia mojawapo ni kudhibiti madawa ya wadudu kwenye mayai yao ambayo mara nyingi ndio yanayoleta usugu. Wanasayansi wa Amerika ya Kaskazini na Kati wametengeneza chombo cha kuyapata mayai ya mbu kwa kutumia vipande viwili ya matairi ya zamani.
Chanzo: Thomson Reuters Foundation