1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nkurunziza awatenga maafisa wa kijeshi wa Kitutsi

Admin.WagnerD31 Desemba 2015

Huku mzozo nchini Burundi ukizidi na kuwa katika hatari ya kuwa wa kikabila ,Rais Pierre Mkuzunziza wa Burundi ametisha kukabiliana na wanajeshi wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika.

https://p.dw.com/p/1HWZ0
Burundi Militärputsch
Picha: Reuters/G. Tomasevic

Rais Pierre Nkurunziza amesema kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika ambacho kimependekezwa kitakiuka katiba ya Burundi ambayo inapinga uingiliaji wowote iwapo kuna serikali inayofanya kazi na hakuna vita kati ya pande mbili.

Rais huyo amesema Burundi itachukulia hatua hiyo kuwa ya uvamizi na ikiwa wanajeshi wa kigeni wataingia nchini humo,watawakabili.

Nkurunziza ambaye ni kutoka kabila la Hutu anaonekana kuwatenga maafisa kijeshi wa kitutsi ambao utiifu wao unatiliwa shaka.Baadhi ya Watusti wanaanza pia kuliasi jeshi na tayari kanali mmoja alitangaza kuunda kundi jipya la waasi wiki iliyopita.

Kuasi kwa Luteni huenda kukazidisha mzozo

Kuasi kwa Luteni kanali Edouard Nshimirima,kumeeneza uvumi kuwa wanajeshi wengine Watusti watamfuata,na kusababisha kuzidi kwa mzozo huo na umwagikaji mkubwa wa damu.

Serikali ya Burundi imelaumu Rwanda ambayo ina makabila sawa na Burundi na inayoongozwa na Rais Mtusi kwa kusajili na kutoa mafunzo kwa waasi wanaompinga Nkurunziza,madai ambayo serikali ya Rwanda imeyakanusha.Zaidi ya watu 800,000 kutoka kabila la Watsusi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawawa nchini Rwanda wakati wa mauwaji wa halaiki 1994.

Muandamanaji akiweka kizuizi wakati wa maandamano ya kumpinga Rais Nkurunziza
Muandamanaji akiweka kizuizi wakati wa maandamano ya kumpinga Rais NkurunzizaPicha: Reuters/G. Tomasevic

Mzozo wa sasa nchini Burundi ulizuka baada ya chama tawala CNDD-FDD kutangaza mwezi Aprili kuwa Nkurunziza awanie muhula wa tatu ,hatua ambayo waangalizi wengi walisema ilikiuka mikataba yote miwili ya amani iliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuwa kinyume pia cha katiba.Mtetezi mmoja maarufu wa haki za binadamu aliliambia shirika la habari la AP mgawanyiko mkubwa wa kikabila wa muda mrefu nchini Burundi ni changamoto kubwa inayoikabili tena nchi hiyo.

Baadhi ya wanachama wanakumbuka mauaji yaliyotokea

Anschaire Nikoyagize,Rais wa muungano wa mashirika ya haki za binadamu amesema wakati serikali madarakani ikihimiza juu ya maridhiano,baadhi ya wanachama wa chama tawala wanakumbuka mauaji yaliyotokea nchini Burundi mwaka 1972 na kukandamizwa wa watutsi walio wachache dhidi ya Wahutu walio wengi chini ya Serikali za kijeshi zilizotawala kati ya miaka ya 1960 na mwisho wa miaka ya 1980.

Jeshi la Burundi liliangaliwa kuwa ufanisi mkubwa wa ule mkataba wa amani wa Arusha wa 2000 kwa kuwaleta pamoja wanajeshi wa Kihutu na wale wa Tutsi na kuwa jeshi moja.

Kwa sasa ufanisi huo unaonekana kuvurugika kutokana na machafuko yamesababisha vifo vya watu 200 na kutishia kuchukua mkondo wa tafauti za kikabila.

Mwandishi:Bernard Maranga/AP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman