Nyota wa michezo walioingia katika siasa
Chama cha Imran Khan nyota matata wa mchezo wa Kriketi, kimeshinda viti vingi katika uchaguzi mkuu wa Pakistan. Khan si mwanamichezo pekee alieingiza mkono ake katika siasa baada ya kustaafu.
Imran Kahn – Waziri Mkuu Mpya wa Pakistan?
Chama cha Imran Khan cha Tehreek-e-Insaf party kimeshinda viti vingi katika uchaguzi wa Pakistan. Miongoni mwa mafanikio ya nyota huyo wa Kriketi ni kuiongoza Pakistan kuchukua ushindi wa kombe la dunia la Kriketi mwaka 1992.
George Weah — Rais wa Liberia
George Weah, anaewakilisha muungano wa mabadiliko ya kidemokrasia, alishinda kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2017. Weah alimshinda makamu wa rais aliekuwepo madarakani Joseph Boakai. Kama mwanakandanda maarufu alichezea timu kama AS Monaco, Paris Saint-Germain na AC Milan. Mwaka 1995 alitajwa kama mwamichezo wa FIFA duniani wa mwaka huo.
Vitali Klitschko — Meya wa Kyiv
Vitali Klitschko alipigana ngumi hadi alipotimiza miaka 40, lakini tayari alikuwa ameshaanza safari nyengine ya maisha katika siasa wakati akitawala katika mchezo wa ndondi. Kwanza alipigana kuwa Meya wa mji mkuu wa Ukraine Kyiv mwaka 2006 , lakini akashinda na kupata nafasi hiyo mwaka 2014 baada ya mageuzi makubwa.
Manny Pacquiao — atakayemrithi Duterte?
Nyota wa ndondi Manny Pacquiao amekuwa mfuasi mkubwa wa rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte tangu alipoachana na ndondi. Duterte amesema zaidi ya mara moja kwamba anatarajia nyota huyo ambae sasa ni seneta kumrithi kama rais wa Ufilipino.
Romario — 'mshindi wa kombe la dunia mwaka 1994/ seneta wa Rio
Romario de Souza Faria alivalia jezi nambari 11 wakati Brazil iliposhinda kombe la dunia mwaka 1994. Ni pele tu na Ronaldo ndio waliofungia mabao mengi timu ya Brazil. Sasa Romario ni seneta katika mji wa Rio de Janeiro,anaewakilisha chama cha kisoshalisti cha rais wa zamani Lula na Dilma Rousseff.
Judy Martz — bingwa wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu na gavana wa Montana
Mwaka 1964 Judy Martz alishinda mbio za mita 1,500 katika mchezo wa kuteleza kwenye barafu na kuwa mwanamke wa kwanza katika jimbo hilo kushindana katika michezo ya Olimpiki. Januari mwaka 2001, alikuwa mwanamke wa kwanza katika jimbo hilo kuchua nafasi ya Ugavana. Alitumikia kipindi kimoja tu hadi mwaka 2005 na hakugombea kipindi cha pili.
Arnold Schwarzenegger — Mchezaji filamu
Watu wengi wanamjua kwa filamu zake maarufu au kama gavana wa zamani wa jimbo la California. Lakini kwa Arnold Schwarzenegger maisha yake yalianzia kama muinua vyuma akiwa na miaka 23. Akawa kijana mdogo kabisa kushinda taji la "Mr Olympia" Gavana wa 38 wa California alichaguliwa mwaka 2003 katika uchaguzi maalum na baadaye akachaguliwa kuwa gavana kamili mwaka 2006.
Bill Bradley — Seneta wa New Jersey
Nyota wa mpira wa kikapu NBA Bill Bradley alikuwa miongoni mwa timu zilizochukua ushindi mwaka 1970 na 1973 katika ushindi uliopatikana katika timu ya Knicks. Lakini pia alisomea historia na kupenda siasa. Kama mwana demokrat alitumikia takriban miongo miwlili kama seneta wa New Jersey.
Sebastian Coe — alishinda medani ya dhahabu miaka ya 90
Enlisting Sebastian Coe alikuwa mwana mapinduzi kwa waingereza wahafidhina wakati wa utawala wa Margaret Thatcher. Mwanariadha, mshindi wa medani ya dhahabu wa mbio za mita 1,500-mwaka 1980 na 1984, Coe alikuwa mbunge mwaka 1992 lakini akapoteza kiti chake katika uchaguzi uliofuata. Sasa anajulikana kwa kazi yake kama balozi katika michezo ya olimpiki ya London na kama rais wa sasa wa IAAF.
Gustav-Adolf Schur — Muendesha baiskeli na msoshalisti
Mtu maarufu wakati wa iliokuwa Ujerumani ya Mashariki, Gustav-Adolf "Täve" Schur alipokuwa na miaka 27 tayari alikuwa mwanachama wa bunge la Mashariki la Ujerumani, alilihudumia kuanzia 1958 hadi lilipovunjwa mwaka 1990, baada ya kuungana kwa Ujerumani mbili ya Magharibi na Mashariki. Wengi wanasema asingepata nafasi katika ukuta maarufu wa waendesha basikeli bora.
Gerald Ford — pia likuwa mwanasoka wakati alipokuwa chuo.
Wengi wanamkumbuka rais wa 38th wa Marekani kama makamu wa rais aliepata nafasi hiyo baada ya kujiuzulu kwa Richard Nixon. Lakini Gerald R. Ford alikuwa pia mchezaji wa kandanda katika chuo kikuu cha Michigan mwaka 1932-34.
Ayrton Senna — aliekosa nafasi nchini Brazil?
Mamia ya raia wa Brazil walimiminika barabarani kuuaga mwili wa Ayrton Senna bingwa wa mashindano wa mbio za magari. Senna alikuwa mtu tofauti sana, alisikitishwa sana na hali ya umasiki nchini mwake Brazil. Wengi waliamini siku moja ataingia katika siasa.