1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUlaya

OECD: Uchumi wa dunia utaimarika kwa ''mwendo wa kobe''

7 Juni 2023

Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) leo limechapisha tathmini ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka ujao likitabiri kwamba utaimarika kwa kiwango kidogo.

https://p.dw.com/p/4SJZu
Frankreich | OECD Hauptsitz in Paris
Picha: Francois Mori/AP Photo/picture alliance

Shiriika hilo limesema ukuaji wa uchumi utakuwa chini ya kiwango cha mwaka uliopita.

Tathmini hiyo inaonesha uchumi wa dunia utakuwa kwa asilimia 2.7 mwaka huu kutokana na matumaini ya kuendelea kupungua kwa Mfumuko wa Bei na kuondolewa kwa vizuizi vya kukabiliana na janga la Corona nchini China.

Hata hivyo OECD imesema ukuaji huo bado ni mdogo ikilinganishwa na asilimia 3.3 iliyorikodiwa mwaka 2022.

Licha ya vizingiti vinavyouandama uchumi wa dunia, OECD imepandisha makadirio yake ya ukuaji wa shughuli za uzalishaji nchini Marekani, China na kwenye kanda ya mataifa yaayotumia sarafu ya euro.