OIC yalaani vita vya Gaza na kuhimiza vikwazo kwa Israel
6 Mei 2024Pia imetoa mwito kwa nchi wanachama kuiwekea vikwazo Israel na kusitisha mara moja kuiuzia silaha nchi hiyo.
Katika tamko la mwisho la mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo uliofanyika nchini Gambia, OIC, imeyarai mataifa 57 wanachama kutumia shinikizo la kidiplomasia, kisiasa na kisheria na kuchukua hatua zozote zitakazosaidia kumaliza kile imekiita "vita vya Israel dhidi ya umma wa Wapalestina."
Pia imetoa mwito wa kupatikana makubaliano ya haraka na ya kudumu ya kusitishwa mapigano.
OIC ambayo iliundwa mwaka 1969 kufuatia kuchomwa moto kwa msikiti wa al-Aqsa, ambao ni moja ya maeneo tukufu kwa waislamu, ina malengo ya kupigania mshikamano miongoni mwa waislamu, kuunga mkono harakati za uhuru wa Palestina na kuyalinda maeneo muhimu ya dini ya kiislamu.