OMANI-BIASHARA NA MAREKANI
11 Machi 2005Matangazo
MUSCAT:
Oman inatumai kufunga mkataba wa biashara na Marekani hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu.Mazungumzo juu ya mkataba huo yanatazamiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii.
Mapatano hayo yanatarajiwa kuimarisha bidhaa za Oman nchini Marekani-amesema Khalfan bin Said al-Rahbi-mkurugenzi katika wizara ya biashara na viwanda nchini Oman.
Saudi Arabia inapinga mapatano ya biashara huru na Marekani ikidai yataweka pingamizi katika kuunganisha uchumi wa nchi zinazotoa mafuta za Ghuba.