1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni ya NATO dhidi ya Libya itaendelea

15 Aprili 2011

Viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Marekani wamesema, kampeni yao ya kijeshi dhidi ya vikosi vya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, itaendelea hadi mashambulio na vitisho vya serikali dhidi ya raia yatakaposita.

https://p.dw.com/p/RI3A
NATO Secretary General Anders Fogh Rasmussen delivers a statement during the informal meeting of the NATO foreign ministers in the Foreign Ministry in Berlin Thursday, April 14, 2011. (AP Photo/Markus Schreiber)
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron (kushoto) na Rais Nicolas Sarkozy wa UfaransaPicha: AP

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na marais wa Ufaransa na Marekani, Nicolas Sarkozy na Barack Obama wameapa kuendelea na kampeni hiyo,mpaka azimio la Umoja wa Mataifa litakapotekelezwa. Viongozi hao wametoa tamshi hilo katika hati ya pamoja iliyochapishwa katika magazeti kadhaa.

Marekani yapinga kupeleka ndege kumshambulia Gadaffi

U.S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton speaks about the situation on the Korean peninsula during a press conference in Beijing, China, Monday, May 24, 2010. Clinton said that North Korea's sinking of South Korean naval ship Cheonan has created a "highly precarious" security situation in the region and that President Barack Obama's administration is working to prevent an escalation of tension that could lead to conflict. (AP Photo/Saul Loeb, Pool)
Waziri wa Nje wa Marekani Hillary ClintonPicha: AP

Lakini katika mkutano wa mawaziri wa nje wa jumuiya ya kujihami NATO mjini Berlin, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, amepinga wito wa Uingereza na Ufaransa kupeleka ndege za kijeshi kushiriki katika operesheni dhidi ya kiongozi wa Libya.

Nae Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen, amekariri kuwa operesheni za kijeshi zinapaswa kuendelea ili kuweza kuwalinda raia wa Libya na kupata suluhisho la kisiasa. Wakati huo huo, Gaddafi alizuru mitaa ya mjini Tripoli, muda mfupi tu baada ya mji mkuu huo mkuu wa Libya kushambuliwa na ndege za kijeshi za NATO.