1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Orban asema yuko tayari kuunga mkono azma ya Mark Rutte NATO

19 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ameeleza utayari wake wa kumuidhinisha Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte kuwa Katibu Mkuu ajaye wa jumuiya ya kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4hDxe
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor OrbanPicha: Attila Volgyi/Xinhua/IMAGO

Hii ni baada ya Rutte anayemaliza muda wake kuhudumu kama Waziri Mkuu wa Uholanzi kutoa hakikisho kwa njia ya maandishi kwamba hatoilazimisha Hungary kushiriki katika mipango mipya ya NATO ya kutoa msaada kwa Ukraine.

Hakikisho hilo linafungua njia kwa Rutte kuchukua nafasi ya Katibu Mkuu ajaye wa NATO.

Soma pia: Hungary yakubali kutopinga msaada wa NATO kwa Ukraine

Pia Rais mpya wa Slovakia Peter Pellegrini amesema nchi yake itamuunga mkono Rutte.

Katika mazungumzo mjini Budapest wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ambaye anatazamiwa kuachia ngazi mwezi Oktoba mwaka huu, alifikia makubaliano na Viktor Orban kuhakikisha kwamba Hungary haitazuia mipango ya msaada kwa Ukraine.