1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Orban atahadharisha Ulaya, China zaelekea vita vya kiuchumi

4 Oktoba 2024

Waziri Mkuu Victor Orban wa Hungary ametahadharisha kwamba Umoja wa Ulaya unaelekea kwenye "vita baridi vya kiuchumi" na China.

https://p.dw.com/p/4lPEy
Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban.
Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban.Picha: Meng Dingbo/Xinhua/dpa/picture alliance

Orban ametowa indhari hiyo wakati viongozi wa kanda hiyo wanajiandaa kupigia kura pendekezo la kuweka ushuru wa forodha kwa magari ya umeme yanayoundwa na China. 

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wataamua leo iwapo wayawekee ushuru wa hadi asilimia 45 katika kipindi cha miaka mitano ijayo magari yote ya umeme yanayoingizwa kwenye kanda hiyo kutoka China, uamuzi ambao unatishia hatua za kujibu mapigo kutoka Beijing. 

Soma zaidi: Je, Orban atafanikisha nia yake ya kutatua mzozo wa Ukraine?

Akizungumza na kituo kimoja cha redio kuhusiana na mipango hiyo, Orban amesema uamuzi wa kuweka ushuru utazusha vita vya kiuchumi na China na itakuwa vigumu kwa bidhaa za Umoja wa Ulaya kupata soko kubwa duniani iwapo biashara ya ulimwengu itagawika baina ya pande mbili zinazohasimiana.

Duru zinasema Ujerumani ambayo ni dola yenye uchumi mkubwa zaidi ndani ya Umoja wa Ulaya itapiga kura kupinga mapendekezo hayo ya kuwekwa ushuru kwa magari ya umeme kutoka China.