1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pakistan yapongezwa kwa zoezi zuri la uchaguzi

10 Februari 2024

Mkuu wa jeshi la Pakistan jenerali Asim Munir, amelipongeza taifa hilo kwa kufanikisha kuandaa uchaguzi wa kitaifa akisema nchi hiyo ilihitaji uongozi thabiti ili kuondoka katika siasa za vurugu na migawanyiko.

https://p.dw.com/p/4cFeN
Pakistan | General Syed Asim Muni
Picha: W.K. Yousufzai/AP/picture alliance

 

Taifa hilo la Kusini mwa Asia lililo na silaha za nyuklia lilishiriki uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi ambapo hadi sasa bado mshindi hajajulikana. Uchaguzi huo unafanyika wakati taifa hilo likijaribu kujikwamua kutoka katika mgogoro wa kiuchumi na vurugu za wanamgambo. 

Licha ya majibu ya uchaguzi kutotolewa, Mawaziri wote wakuu wa zamani Nawaz Sharif na Imran Khan wamejitangaza washindi jana Ijumaa. 

Washirika wa Imran Khan waongoza uchaguzi Pakistan

Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya kwa pamoja walielezea wasiwasi wao kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi wakitoa wito wa uchunguzi wa madai ya udanganyifu.