1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Palestina yaahidiwa dola bilioni 7.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdCv

Paris.

Mataifa fadhili yameahidi kuipatia mamlaka ya Palestina dola bilioni 7.4 katika mkutano wa siku moja mjini Paris. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema kuwa fedha hizo ni tumaini la mwisho kuiokoa serikali ya Palestina kuweza kufilisika.

Waziri mkuu wa Palestina Salam Fayyad kimsingi alitoa ombi la kiasi cha dola bilioni 5.6 kusaidia kutekeleza mipango ya kuendeleza uchumi imara kwa ajili ya taifa la baadaye la Palestina.

Kundi la Hamas hata hivyo limeueleza mkutano huo kuwa ni njama hatari ya kuwagawa Wapalestina.