SiasaSudan
Pande hasimu Sudan zatumia njaa kama silaha - Wataalamu UN
27 Juni 2024Matangazo
Kauli hiyo inatolewa wakati wasiwasi ukiongezeka kuhusiana na kuenea kwa baa la njaa nchini humo. Watalaamu hao wamesema vikosi vya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF wanatumia chakula kama silaha na kuwaacha raia wateseke kwa njaa.
Wanasema kiwango cha njaa na watu kupoteza makaazi yao kinachoonekana nchini Sudan hakijawahi kushuhudiwa.
Mapigano yaliyodumu kwa miezi 14 yamewauwa zaidi ya watu 14,000 na kuwajeruhi wengine 33,000, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, lakini wanaharakati wa haki wanasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Zaidi ya watu milioni 11 wamelazimika kuyakimbia makaazi yao.