Papa asema 'mauaji ya kimbari' yalifanyika Canada
30 Julai 2022Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, amekiri leo kuwa jaribio la kuondoa utamaduni wa jamii ya watu wa asili nchini Canada kupitia mfumo wa shule za Kanisa hilo lilikuwa sawa na mauaji ya kimbari.
Soma pia: Papa Francis afanya maombi ya uponyaji kwa ukoloni 'mbaya' nchini Canada
Akizungumza na waandishi habari akiwa njiani kurudi nyumbani akitokea Canada, Papa Francis amesema hakutumia neno hilo wakati wa ziara yake lakini aliomba msamahakwa sababu mchakato huo ulikuwa mauaji ya kimbari.
Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1800 hadi 1990, serikali ya Canada ilipeleka karibu watoto 150,000 kwenye shule 139 zinazoendeshwa na Kanisa, ambako walitengwa na familia zao, lugha na utamaduni.
Wengi walidhalilishwa kimwili na kingono, na maelfu wanaaminika kufa kwa magonjwa, utapiamlo au utelekezwaji.
Soma pia: Papa Francis aomba radhi kwa makosa ya Kanisa nchini Canada
Tangu Mei 2021, zaidi ya makaburi 1,300 yamegundulika kwenye maeneo zilikokuwa shule hizo, na kuzusha mshtuko nchini Canada, ambao ilianzataratibu kukiri kuhusu matukio hayo ya kusikitisha ya historia yake.
Tangu mwaka jana mamia ya mabaki ya Watoto waliozikwa kwenye makaburi ambayo hayakujulikana yaligundulika katika maeneo ya shule za zamani, na kusababisha mshtuko kote nchini humo.
Viongozi wa kikabila waliokutana na Papa walikubali msamaha wa kanisa kuhusu maovu hayo lakini wakasema watu wao wanamtarajia achukua hatua zaidi kuelekea kuwapa fidia.
Papa adokeza kuhusu kustaafu
Pia akiwa njiani, Papa Francis ameelezea ziara ya Canada kuwa mtihani kwa afya yake inayozorota akikiri kuwa hawezi tena kusafiri katika uwezo saw ana angalau anahitaji kupunguza safari. Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 85 anatatizwa na maumivu ya misuli ya goti ambayo yamemlazimu kutumia kiti cha walemavu kwa sehemu kubwa ya ziara yake.
Ingawa hakuwa amewaza kabla kuhusu kustaafu, papa amewaambia waandishi Habari kuwa hakuna kitu kibaya kwa yee kuwachia ngazi.
"Unaweza kumbadilisha papa,” amesema. "Nadhani katika umri wangu na hizi changamoto, napaswa kuhifadhi nguvu zangu ili kulitumikia kanisa, au kinyume chake kufikiri kuhusu uwezekano wa kuachia ngazi."
Maumivu ya goti yalimfanya kuifuta ziara yake ya Afrika katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai.
rmt/sri (AP, AFP, Reuters)