Papa azungumzia juu ya machafuko hotuba yake ya kila mwaka
8 Januari 2024Papa Francis amezungumzia masuala kadhaa ikiwemo vita, uhamiaji, mzozo wa mabadiliko ya tabianchi na uundaji wa silaha za maangamizi.
Kuhusu vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine pamoja na mzozo wa Israel na kundi la Hamas huko Gaza, Papa Francis amesema mashambulizi yasiyobagua kwenye uwanja wa vita ni uhalifu kwa sababu ni kinyume na sheria ya kimataifa.
Soma pia: Papa ahimiza huruma kwa wanawake na watoto wanaonyanyasika
Kiongozi huyo wa kiroho aligusia kwa kirefu mzozo wa Mashariki ya Kati akirejea msimamo wa kanisa juu ya suluhisho la kuundwa madola mawili kama njia ya kumaliza uhasama kati ya Israel na Palestina.
Papa Francis pia amekosoa wimbi la mapinduzi barani Afrika na chaguzi kwenye baadhi ya nchi za bara hilo alizosema ziligubikwa na "rushwa, vitisho na vurugu."