JamiiMongolia
Papa Francis aisifu Mongolia kwa amani na uhuru wa dini
2 Septemba 2023Matangazo
Katika hotuba yake mbele ya viongozi wa serikali na wawakilishi wa makundi ya kiraia wa Mongolia, Papa Francis amesema nchi hiyo ina wajibu mkubwa barani Asia kutokana na misingi yake ya kuheshimu haki za binadamu na diplomasia.
Miongoni mwa masuala aliyotaja ni pamoja na uamuzi wa Mongolia kufuta adhabu ya kifo, ustahamilivu wa kidini na utunzaji mazingira.
Hotuba hiyo ya Baba Mtakatifu Francis ndiyo shughuli ya kwanza kuifanya tangu alipowasili kwenye mji mkuu Ulaanbaatar siku ya Ijumaa kwa ziara ya siku tatu nchini Mongolia, taifa lenye kiasi waumini 1,500 pekee wa kikatoliki.
Mapema asubuhi alilakiwa kwa hafla ya heshima iliyohuhduriwa na mamia ya waumini ikiwemo kutoka China na Taiwan.