1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ajitolea kumpa hifadhi Aung San Suu Kyi

24 Septemba 2024

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amejitolea kumpa hifadhi Vatican kiongozi wa zamani wa Myanmar Aung San Suu Kyi anayetumikia kifungo nchini Myanmar.

https://p.dw.com/p/4l2Zn
Kiongozi wa zamani wa Myanmar Aung San Suu Kyi
Kiongozi wa zamani wa Myanmar Aung San Suu Kyi Picha: Nyein Chan Naing/AP/picture alliance

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amejitolea kumpa hifadhi Vatican kiongozi wa zamani wa Myanmar Aung San Suu Kyi anayetumikia kifungo nchini Myanmar. Haya yameripotiwa leo na vyombo vya habari vya Italia.

Kulingana na mazungumzo wakati wa mikutano na mapadre wa shirika la kanisa katoliki la Jesuits huko Asia wakati wa ziara yake mapema mwezi huu, papa Francis alisema kuwa aliomba kuachiwa huru kwa Suu Kyi na kupendekeza kwa Vatican kumpa hifadhi.

Gazeti la The Corriere della Sera, lilichapisha makala ya kasisi wa Italia Antonio Spadaro akitoa dondoo kutoka kwa mikutano hiyo ya faragha iliyofanyika Indonesia, Timor Mashariki na Singapore kati ya Septemba 2 na 13

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki alinukuliwa akisema hawawezi kunyamaza kuhusu hali ilivyo Myanmar kwasasa na kwamba lazima wachukuwe hatua.

Suu Kyi, mwenye umri wa miaka 78, anatumikia kifungo cha miaka 27 gerezani kwa mashtaka yanayojumuisha ufisadi pamoja na kutoheshimu vizuizi vya janga la Uviko -19