1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis awakemea unyanyasaji wa kingono Ureno

3 Agosti 2023

Papa Francis amewakemea viongozi wa Kanisa Katoliki la Ureno kwa kashfa ya unyanyasaji wa kingono unaowahusisha mapadri.

https://p.dw.com/p/4Uiik
Papst Franziskus Treffen mit Marcelo Rebelo de Sousa in Lissabon
Picha: Antonio Oedro Santos/REUTERS

Akizungumza wakati akianza ziara yake katika nchi hiyo ya Ulaya, Kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni amesema vitendo vya mapadri hao vimechangia kuwafukuza kanisani waumini na akawaamuru viongozi wa kanisa Katoliki kubadili mienendo yao na kuwajali zaidi wahanga wa maovu hayo.

Soma pia: Papa Francis akemea kashfa ya unyanyasaji wa kingono Ureno

Jopo la wataalamu lililoteuliwa na kanisa la Ureno liliripoti Februari kuwa makasisi na viongozi wengine wa kanisa huenda waliwadhalilisha karibu wavulana na wasichana 4,815 tangu mwaka wa 1950.

Francis yuko Lisbon kushiriki Siku ya Vijana Ulimwenguni, tamasha la kikatoliki la siku tano lililoanzishwa na Mtume Paul John II katika miaka ya 1980 ili kutia nguvu kizazi kijacho cha Wakatoliki katika imani yao.

Ni tamasha la kwanza kufanyika tangu kuzuka janga la UVIKO-19.