1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis akutana na viongozi wa dini ya kiyahudi

6 Novemba 2023

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis,amekutana na viongozi wa kiyahudi wa Ulaya na kulaani chuki dhidi ya wayahudi,vita pamoja na ugaidi kupitia hotuba yake aliyoshindwa kuisoma kutokana na sababu za kiafya.

https://p.dw.com/p/4YTfI
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis.
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis.Picha: Vatican Media/REUTERS

 Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema shughuli za kiongozi huyo zinaendelea kama kawaida licha ya kuugua homa.

Soma pia:Jeshi la Israel lashambulia maeneo 450 katika Gaza

Katika hotuba yake iliyoandaliwa mapema Papa Francis amesema fikra na mawazo yake yako katika kila kitu kilichotokea wiki kadhaa zilizopita,akimaanisha tukio la Oktoba 7 la shambulio la Hamas dhidi ya Israel lililohusisha pia utekaji nyara wa Waisrael.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW