1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Papa Francis alaani visa vya kuchomwa Quran Tukufu

3 Julai 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amelaani kwa matamshi makali vitendo vya kuchomwa kitabu kitakatifu kwa Waislamu, Qur'an.

https://p.dw.com/p/4TLNu
KEIN Titelbild! Schlechte Bildqualität!  Reportage Bangladesch Freiheitskämpfer
Picha:

Papa Francis pia ametoa mwito wa kuheshimiwa kwa vitabu vitakatifu vya dini kama njia ya kuonesha heshima kwa watu wanaoviamini. Katika mahojiano na gazeti la Al-Ittihad linalochapishwa huko Falme za Kiarabu, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema amechukizwa na matendo hayo na kupinga juhudi zozote za kuruhusu matukio hayo kuwa sehemu ya uhuru wa maoni.

Matamshi ya Papa Francis yanafuatia kitendo cha wiki iliyopita ambapo mtu mmoja aliichoma Quran Tukufu kwenye mji mkuu wa Sweden, Stockholm, na kuzusha hasira kutoka mataifa kadhaa duniani.

Soma zaidi: Iran yasitisha kumpeleka balozi wake nchini Sweden kupinga kitendo cha kuchomwa kwa Quran

Ingawa mamlaka za Sweden zimekuwa zikikataa maombi ya maandamano ya kuipinga Quran, mahakama za nchi hiyo zimepinga katazo hilo zikisema zinaingilia uhuru wa watu kujieleza.