1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMongolia

Papa Francis awasili Mongolia katika ziara yake ya kwanza

Sylvia Mwehozi
1 Septemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili siku ya Ijumaa nchini Mongolia katika ziara yake ya kwanza ya kipapa katika taifa hilo la kanda ya Asia.

https://p.dw.com/p/4Vpiv
Papst Franziskus besucht Mongolei
Picha: Vatican Media/Reuters

Ziara ya Papa katika taifa hilo lenye waumini wengi wa Kibudha ni ishara ya kuunga mkono jamii ndogo ya Wakatoliki wapatao 1,400. Ametuma ujumbe wa amani na mshikamano kwa taifa jirani la China ili kukuza mahusiano.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye ndege,  Papa Francis   amesema: 

"Kwenda Mongolia kunamaanisha kutembelea idadi ndogo ya watu katika nchi kubwa. Mongolia inaonekana kutokuwa na kikomo na ina wakaazi wachache lakini yenye utamaduni mkubwa".

Ziara ya Francis pia ni mkakati wa kuimarisha uhusiano wa Vatican na nchi jirani na Mongolia yaani China na Urusi. China haina uhusiano rasmi na Vatican.