Papa Francis kuzuru Kongo na Sudan Kusini wiki ijayo
26 Januari 2023Kiongozi huyo mwenye miaka 86 alilazimika kuahirisha ziara hiyo mwaka jana baada ya kupata matatizo ya goti na safari hiyo kupangwa upya.
Papa Francis alizuru kwa mara ya kwanza Afrika, Novemba 2015, kwa kuzitembelea Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako aliziomba pande zinazohasimiana kuacha mapigano huku akiisifu Afrika kuwa ni bara la matumaini.
Aprili mwaka 2017, Papa Francis alizuru Misri kwa siku mbili kuonyesha kuwaunga mkono waumini wa madhehebu ya wakristo wa Coptic, walio wachache, ambao wengi wao wapo katika ukanda wa Mashariki ya Kati na wanaokabiliwa na kitisho cha mashambulizi makubwa ya kila mara.
Mwaka 2019, alizuru Morocco kufuatia mwaliko wa Mfalme Mohammed VI ambako alisisitizia umuhimu wa mazungumzo na Waislamu, na mwaka 2019, akiitembelea Msumbiji, Madagascar na Maurutius.