1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ziarani Marseille kujadili mzozo wa wahamiaji

22 Septemba 2023

Mkuu wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis, anaelekea Marseille kwa ziara ya siku mbili inayolenga kuangazia suala la uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4Wgcj
Papa Francis
Papa FrancisPicha: Vatican Media/REUTERS

Mkuu wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis, anaelekea Marseille kwa ziara ya siku mbili inayolenga kuangazia suala la uhamiaji na ujumbe wa uvumilivu huku kukiwa na mjadala mkali kuhusu namna Ulaya inavyowashughulikia wahamiaji wanaotafuta hifadhi.Waziri Mkuu wa Italia aapa hatua kali kuzuia wahamiaji

Hali ya watu kukata tamaa na kuwasababisha kutafuta maisha mapya nchi za nje huku wakihatarisha maisha yao baharini, imekuwa mada kuu kwa Papa Francis mwenye umri wa miaka 86, katika muongo mmoja akiwa Papa.

Lakini ziara yake katika mji wa bandari wa Ufaransa Marseille, kushiriki mkutano wa maaskofu wa Kikatoliki wa eneo la Mediterania na vijana, inamweka katikati ya dhoruba ya kisiasa.

Ongezeko la wahamiaji kutoka kaskazini mwa Afrika waliowasili kisiwani Lampedusa wiki iliyopita, kulizusha ghadhabu nchini Italia na kwingineko.