1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa kukutana na wakimbizi Hungary

29 Aprili 2023

Papa Francis, ambae yuko ziarani kwa siku tatu nchini Hungary, leo hii anatarajiwa kukutana na wakimbizi wa Ukraine

https://p.dw.com/p/4Qi4q
Ungarn | Papst Franzisus in Budapest
Picha: Denes Erdos/AP/picture alliance

Papa Francis, ambae yuko ziarani kwa siku tatu nchini Hungary, leo hii anatarajiwa kukutana na wakimbizi wa Ukraine na wanaotoka sehemu nyingine katika kipindi hiki ambacho wengi wao nchini humo wako katika mazingira magumu kutokana na sera za Waziri Mkuu Viktor Orban.Baada ya kuwasili hapo jana Papa mwenye umri wa miaka 86, katika hotuba yake ya kwanza kwa Orban na maafisa wengine wa serikali alisisitiza haja ya uwazi kwa wengine huku akionya dhidi ya kujitenga.Serikali ya Hungary tofauti na msimamo wake wa awali wa kupinga wakimbizi, sasa imewaruhusu wakimbizi wa Ukraine kuingia katika mipaka ya ardhi yake. Lakini wanaharakati wanasema hakuna mfumo wa kuwasaidia wakimbizi, wakati huu Waziri Mkuu Orban akiendelea kudumisha uhusiano wake na serikali ya Urusi. Hatua hiyo, imekuwa ikiwakasirisha wa watu wa Ukraine.